Tayammum imewekwa kwa ajili ya hadathi na si najisi

Lau mtu atakuwa nchi kavu na nguo yake ikapatwa na najisi na hana kitu cha kuiondoshea najisi hiyo. Je, afanye Tayammum ili aswali kwenye nguo hii? Hapana asifanye Tayammum. Hali kadhalika lau mguu, mkono au muundi wake utapatwa na najisi na yuko nchi kavu na hana kitu cha kuondoshea najisi hiyo na anataka kuswali. Je, afanye Tayammum? Hapana asifanye Tayammum. Kwa kuwa Tayammum imewekwa kwa ajili ya kutwahirisha hadathi tu. Tayammum haitumiwi katika najisi. Kwa kuwa najisi ni uchafu uliosimama kwa dhati yake na kutwahirishwa kwake ni kwa kuiondosha pale inapowezekana. Ikiwa haiwezekani itabaki mpaka pale itapowezekana kuiondosha. Na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/368)
  • Imechapishwa: 16/05/2023