Swalah ya Ishraaq ndio swalah ya Dhuhaa

Swali: Je, Sunnah ya Ishraaq (الإشراق) inaingia ndani ya Sunnah ya Dhuhaa?

Jibu: Ndio. Inatosha kutokana na Sunnah ya Dhuhaa. Sunnah ni kuanzia pale jua linaposimama kiasi cha mkuki mpaka jua lisimame. Lakini bora ya wakati wake ni pale jua linapokuwa kali zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya wingi wenye kurejea ( الأوابين) ni pale joto linakuwa kali zaidi.”

Joto linapokuwa kali zaidi ndio wakati bora zaidi. Lakini ni sawa pia mtu akiiswali mapema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22590/هل-تدخل-سنة-الاشراق-في-سنة-الضحى
  • Imechapishwa: 07/07/2023