Swali: Mtu akiwa ni msafiri na akasikia adhaana aswali na mkusanyiko?

Jibu: Ni sawa ikiwa ni wepesi. Vinginevyo yuko na safari ikiwa anachelea anaotangamana nao au kitu kitachompita. Katika hali hiyo aendelee na safari na aswali njiani.

Swali: Akikosa swalah ya mkusanyiko kisha akarudi nyumbani – je, aiswali kwa kufupisha?

Jibu: Aswali kwa kufupisha Rak´ah mbili. Hilo linahusu Dhuhr, ´Aswr na ´Ishaa. Akiswali na wengine basi aiswali Rak´ah nne.

Swali: Je, analazimika kuswali na mkusanyiko asiposikia adhaana?

Jibu: Analazimika akiwa yuko peke yake. Lakini akiwa na wengine ni mwenye khiyari; wakitaka wataswali wenyewe hali ya kufupisha na wakitaka wataswali na mkusanyiko na wengine na hivyo watakamilisha Rak´ah nne.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22551/هل-تجب-الجماعة-للمسافر-لو-سمع-النداء
  • Imechapishwa: 07/07/2023