Ni lazima kuwa na wudhuu´ kwa ajili ya kukaa msikitini?

Swali: Mwenye kukaa msikitini kwa ajili ya kuhudhuria swalah au mfano wake kisha wudhuu´ wake ukachenguka – je, analazima kutawadha tena papohapo?

Jibu: Si lazima. Lakini asiketi msikitini akiwa na janaba. Lakini akiwa hana janaba – hata kama hana twahara – akae chini na kusikiliza darsa na faida hata kama hana twahara. Isipokuwa mwenye janaba peke yake. Haifai kwa mwenye janaba kukaa mpaka kwanza akoge.

Swali: Akirudi aswali Rak´ah mbili?

Jibu: Akirudi aswali Rak´ah mbili ambazo ni Sunnah ya wudhuu´ na swalah ya mamkuzi ya msikiti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22591/هل-يلزم-الوضوء-للجلوس-بالمسجد
  • Imechapishwa: 07/07/2023