Swali: Mtu atoe swadaqah kwa pesa inayotokana na kupiga chuku?

Jibu: Aitolee swadaqah.

Swali: Je, si ni pesa yenye kudharauliwa?

Jibu: Hapana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kutoa swadaqah. Alimpa Abu Twayyibah malipo ya kupiga chuku. Lakini ni chumo baya na lenye kutwezwa. Aitolee swadaqah kwa sababu ni pesa yake. Ni pato lenye kudharauliwa. Kila mmoja anatoa swadaqah kutegemea na kile alichonacho. Ambaye hamiliki isipokuwa tende mbaya aitoe swadaqah. Ambaye anamiliki nguo zisizo nzuri atoe swadaqah. Kila mmoja kutegemea na hali yake:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21684/هل-تجوز-الصدقة-من-مال-الحجام
  • Imechapishwa: 11/09/2022