Swali: Mwenye kufa ilihali bado anaendelea juu ya shirki ndogo anaingia ndani ya matakwa ya Allaah?

Jibu: Udhahiri ni kwamba hatosamehewa isipokuwa kwa moja ya mambo mawili:

1 – Matendo yake mazuri yawe na uzito zaidi.

2 – Kuadhibiwa kwa kiwango cha shirki yake.

Ni kama mwenye madhambi makubwa asipotubia yuko chini ya matakwa ya Allaah. Lakini huyu haingii chini ya utashi wa Allaah kwa sababu amefanya shirki. Yuko khatarini. Ima akaadhibiwa au akasamehewa matendo yake mema yasipokuwa na uzito zaidi.

Swali: Ni yepi maoni ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah juu ya hili?

Jibu: Sijui. Sijaona chochote juu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21683/ما-حكم-من-مات-مصرا-على-الشرك-الاصغر
  • Imechapishwa: 11/09/2022