Suurah fupifupi katika Tarawiyh

Swali: Baadhi ya maimamu wanasoma Suurah fupifupi na wanafupika juu ya jambo hilo katika swalah ya Tarawiyh na hawakhitimishi Qur-aan kabisa. Ni ipi hukumu ya kitendo hicho?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Kila mmoja anasoma kile alichomsahilishia Allaah. Ni mamoja amesoma Qur-aan yote, amesoma zile Suurah za katikati au amesoma zile Suurah alizohifadhi. Hapana vibaya kwa yote hayo. Lakini bora zaidi asome Qur-aan yote ikiwezekana ijapo ni kwa kutazamia ndani ya msahafu. Anaweza kuweka kiti pembeni yake na akasoma ndani ya msahafu. Anapotaka kurukuu na kusujudu akaiweka juu ya kiti na anaposimama akasoma ndani yake. Dhakwaan, mtumwa wa ´Aaishah aliyemwacha huru, alikuwa akiwaswalisha katika Ramadhaan kwa kutazamia ndani ya msahafu. Maoni ya sawa ni kwamba hapana vibaya kufanya hivo. Hili ndio la sawa ya kwamba hakuna neno akasoma ndani ya msahafu. Hapana vibaya vilevile akiacha kufanya hivo na akawasomea sehemu katika juzu ya ´Amma au sehemu katika juzu jingine. Kuna wasaa katika jambo hili. Si lazima kusoma Qur-aan yote. Hapana vibaya akiwaswalisha ndani ya Ramadhaan kwa sehemu tu katika Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/8604/حكم-القراءة-في-التراويح-بقصار-السور-وعدم-الختم
  • Imechapishwa: 05/04/2023