Kusoma kimyakimya au kwa sauti ya juu katika swalah ya usiku?

Swali: Je, swalah ya usiku na kisomo ndani yake inakuwa kimyakimya au kwa sauti ya juu?

Jibu: Swalah ya usiku ni kwa sauti ya juu. Hata hivyo hapana neno akisoma kimyakimya. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisoma kimyakimya na alisoma kwa sauti ya juu. Akiona manufaa ni katika kusoma kimyakimya atafanya hivo, na akiona manufaa ni katika kusoma kwa sauti ya juu atafanya hivo. Ijapo kusoma kwa sauti ya juu ndio bora zaidi ikiwezekana. Na ikiwa kusoma kimyakimya ndio moyo wake unaingiwa na unyenyekevu zaidi basi hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9812/حكم-الجهر-والاسرار-في-صلاة-الليل
  • Imechapishwa: 05/04/2023