Swali: Ni upi wakati wa swalah ya Tahajjud? Wakati wake unaanza lini na unaisha lini?

Jibu: Unaanza baada ya swalah ya ´Ishaa na unaisha kwa kuchomoza kwa alfajiri. Huu ndio wakati wa Tahajjud. Watu wakishaswali ´Ishaa basi umeingia wakati wa Tahajjud mpaka kuingia kwa alfajiri. Akiswali Witr mwanzoni, katikati au mwishoni mwa usiku yote ni sawa. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ

“Amka sehemu ya usiku na uswali ni ziada ya sunnah kwako.”[1]

يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ قُمِ اللَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا

“Ee uliyejifunika! Simama usiku [uswali] kucha isipokuwa [muda] mdogo tu.”[2]

Sunnah ni kusimama usiku kuanzia pale inapomalizwa swalah ya ´Ishaa mpaka kuchomoza kwa alfajiri ijapo kwa Rak´ah moja tu. Lakini akiswali Rak´ah tatu, tano au zaidi na anatoa Tasliym kila baada ya Rak´ah mbili ndio Sunnah. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 17:79

[2] 73:01-02

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9342/متى-يبدا-وقت-صلاة-التهجد-ومتى-ينتهي
  • Imechapishwa: 05/04/2023