Swali: Watu wanazumgumzia sana kuhusu wanawake kuswali Tahajjud au Tarawiyh misikitini. Je, una cha kuzungumza juu ya hili?

Jibu: Hapana neno wanawake kuswali pamoja na waislamu misikitini. Lakini watilie umuhimu kujisitiri, kujichunga kutokana na fitina na kutoweka manukato wanayotembea nayo masokoni. Wajihadhari kutokana na manukato na kuonyesha mapambo. Bali awe mwenye kujisitiri na mwenye kuvaa Hijaab na mwenye kujiepusha na sababu za fitina. Vinginevyo nyumbani kwake ndio bora kwake. Nyumba yake ni bora na kheri kwake. Lakini haja ikipelekea yeye kutoka kwa sababu anahisi uvivu kukaa nyumbani kwake, anataka kusikiliza mawaidha na ukumbusho, hapana vibaya kufanya hivo. Lakini kwa sharti zifuatazo: kujihifadhi, kujitunza, kujisitiri, kujiepusha na sababu za fitina si kwa upande wa manukato, mavazi wala kuonyesha mapambo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/7235/حكم-خروج-النساء-لصلاة-التراويح
  • Imechapishwa: 04/04/2023