Makatazo ya kuswali Witr mbili usiku mmoja

Swali: Je, inafaa nikaswali Witr mbili katika usiku mmoja?

Jibu: Haitakikani kwa yeyote kuswali Witr mbili katika usiku mmoja. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”[1]

“Ifanye swalah yenu ya mwisho usiku ni Witr.”[2]

 “Anayechelea kutoamka mwisho mwa usiku basi aamche mwanzoni mwake, na anayetaraji kuamka mwishoni mwake basi aswali Witr mwishoni mwa usiku. Hakika swalah mwishoni mwa usiku ni yenye kushuhudiwa – na hilo ndio bora.”[3]

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Ikiwezekana kwa muislamu kuiswali Tahajjud yake mwishoni mwa usiku, basi aimalize swalah yake kwa Rak´ah moja awitirishe kwayo. Na asiyeweza hilo basi aswali Witr mwanzoni mwa usiku. Allaah akimfanyia wepesi kuamka kuswali kisimamo cha usiku mwishoni mwa usiku, basi ataswali shafwa awezavyo Rak´ah mbilimbili na asirudi kuleta Witr. Ile Witr yake ya kwanza inatosha kutokana na Hadiyth iliotangulia pale ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

“Hakuna Witr mbili katika usiku mmoja.”

[1] at-Tirmidhiy (432) na an-Nasaa´iy (1661).

[2] al-Bukhaariy (943) na Muslim (1245).

[3] Muslim (1255).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/310)
  • Imechapishwa: 04/04/2023