Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anasahau du´aa ya Qunuut katika swalah ya Witr na akasujudu kabla ya kuiomba? Je, inaungwa na sijda ya kusahau?

Jibu: Hakuna kinachomlazimu. Mwenye kusahau Qunuut ya Witr hakuna kinachomlazimu. Halazimiki kuleta sijda ya kusahau. Hapana neno endapo atasujudu. Lakini haimlazimu. Qunuut ya Witr inapendeza na sio lazima. Akiiacha baadhi ya nyakati kwa makusudi hapana neno kama walivofanya baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Jambo ni lenye wasaa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6557/حكم-من-نسي-قنوت-الوتر
  • Imechapishwa: 04/04/2023