Mwanamke kunyanyua sauti yake katika du´aa ya Qunuut

Swali: Mimi huswali ´Ishaa kisha baada yake nikaswali Rak´ah mbili halafu nikaswali Rak´ah mbili kwa Tasliym mbili, kisha nikaswali Rak´ah moja, nikanyanyua juu mikono yangu, nikaomba du´aa kwa kupandisha sauti juu kidogo. Je, ninayoyafanya ni sahihi?

Jibu: Ndio, yote ni sahihi na mazuri. Kupandisha sauti ni kama tulivyotangulia kusema. Ikiwa mbele yako, ee dada muulizaji, hakuna mwanamme wa kando, basi hapana vibaya kwa kiasi cha kufunguka kifua chako, kupata uchangamfu, kutikisika moyo wako na kupata unyenyekevu. Lakini ikiwa mbele yako kuna mwanamme wa kando basi kuishusha ndio aula na bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12139/حكم-رفع-المراة-صوتها-في-دعاء-الوتر
  • Imechapishwa: 04/04/2023