Si lazima kusoma Qunuut katika Witr

Swali: Je, ni lazima kuleta Qunuut wakati wa kuswali swalah ya Witr? Je, imepokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliswali Witr bila Qunuut?

Jibu: Qunuut si jambo la lazima. Qunuut ni kitu kinapendeza. Witr inapendeza na Qunuut inapendeza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimfunza nayo al-Hasan bin ´Aliy. Kwa hivyo ni kitu kinapendeza na si faradhi. Hatujui kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alidumu kuleta Qunuut kama ambavo hatujui kuwa mara aliacha na mara alifanya. Hata hivyo Maswahabah mara walifanya na mara nyingine waliacha. Ubayy bin Ka´b wakati alipokuwa anawaswalisha watu katika zama za ´Umar mara alikuwa akiileta na wakati mwingine akiiacha. Kwa hivyo hapana vibaya kuiacha. Ni jambo linalopendeza. Hapana neno akiiacha baadhi ya nyakati.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/5273/هل-يلزم-القنوت-في-صلاة-الوتر