Siku sita za Shawwaal kwa anayedaiwa Ramadhaan

Swali: Je, inafaa kufunga siku sita za Shawwaal ilihali nadaiwa swawm ya mwezi wa Ramadhaan? Nina shauku kubwa ya kufanya hivo lakini siwezi kulipa kutokana na mambo fulani ikiwa ni pamoja na masomo, maisha ya kindoa na mengineyo. Naomba maelekezo na Allaah akujaze kheri.

Jibu: Kilicho cha lazima ni kulipa deni kwanza kabla ya kuanza kufunga siku sita. Mtu asifunge siku sita za Shawwaal isipokuwa baada ya kulipa deni la Ramadhaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia [siku] sita za Shawwaal, basi anakuwa kama amefunga mwaka mzima.”[1]

Ambaye anadaiwa Ramadhaan hajafunga na akaimaliza Ramadhaan. Amebakiza siku. Siku sita hizi zinaifuatia Ramadhaan. Kwa hivyo ni lazima kwa mtu kulipa deni kwanza ndio afunge siku sita.

[1] Muslim (1164).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9766/حكم-صيام-الست-من-شوال-لمن-كان-عليه-قضاء
  • Imechapishwa: 05/05/2022