Wakati wa kufunga siku sita za Shawwaal

Swali: Nikifungua katika swawm ya siku sita za Shawwaal kisha nikataka kuendelea kuzifunga katika mwezi huohuo – ni lini inaanza? Je, kuna tarehe maalum?

Jibu: Shawwaal yote ni wakati wa kufunga. Bora ni mtu kuiharakisha kabla ya kupatwa na vitu vya kumzuia. Ni mamoja kwa kufululiza au kwa kuachanisha. Ni sawa endapo atafunga mwishoni mwa mwezi au katikati yake. Suala hili ni lenye wasaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia [siku] sita za Shawwaal, basi anakuwa kama amefunga mwaka mzima.”[1]

Hakuweka kikomo mwanzoni mwake, katikati yake wala mwishoni mwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala) amesema:

وَعَجِلْتُ إِلَيْكَ رَبِّ لِتَرْضَىٰ

“Na nimeharakiza kukujia Mola wangu ili uridhike.”[2]

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ

“Kimbilieni msamaha kutoka kwa Mola wenu.”[3]

فَاسْتَبِقُوا الْخَيْرَاتِ

”Basi shindaneni katika mambo ya kheri.”[4]

[1] Muslim (1164).

[2] 20:84

[3] 03:133

[4] 02:148

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15599/وقت-صيام-الست-من-شوال
  • Imechapishwa: 05/05/2022