Sifa nne za swalah tofauti na nguzo zingine

Swalah ina mambo manne:

1 – Haikufaradhishwa kamazakaah, swawm na hajj. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliichukua moja kwa moja kutoka kwa Allaah (Ta´ala).

2 –Mahali. Alipoichukua ilikuwa ndio sehemu ya juu kabisa alipofika binadamu. Kwa msemo mwingine haikufaradhishwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yuko katika ardhi.

3 – Wakati. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliichukua katika wakati mtukufu kabisa ambao ni usiku wa Mi´raaj.

4 – Haikufaradhishwa swalah moja. Bali kulifaradhishwa swalah khamsini. Hili linaonyesha kuwa Allaah anaipenda sana na kwamba anampenda mja wake awe daima ni mwenye kushughulika nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/356 )
  • Imechapishwa: 09/05/2023