22. Wakati chakula na ukimya vinakuwaBid´ah

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoa Khutbah tahamaki akamuona bwana mmoja amesimama akisema: Akaulizia juu yake ambapo wakasema: “Abu Israaiyl ameweka nadhiri ya kusimama na kutoketi chini, kutokaa chini ya kivuli wala kutozungumza. Aidha ya kufunga.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mwamrisheniazungumze, akae chini ya kivuli, aketi chini na atimizeswawm yake.”[1]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kunyamaza daima ni jambo la kizushi lililokatazwa. Vivyo hivyo kujizuia kula mkate, nyama na kunywa maji; ni mambo ya kizushi yenye kusimangwa.”[2]

Amesema tena kuhusiana na Hadiyth hiyo:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha kufunga peke yake, kwa sababu Allaah (Ta´ala) anapenda ´ibaadah ya kufunga. Yaliyosalia sio ´ibaadah ijapo atafikiri mwenye kufikiri kuwa yanamkurubisha kwa Allaah.”[3]

Qays bin AbiyHaazim amesema:

“Abu Bakr aliingia kwa mwanamke mmoja anayetoka Ahmas akiitwa Zaynab. Akamuona haongei ambapo akasema: “Kwa nini hazungumzi?” Wakasema: “Amehiji hali ya kunyamaza.” Akamwambia mwanamke yule: “Zungumza. Si halali kwako. Haya ni miongoni mwa matendo kabla ya kuja Uislamu.”[4]

ash-Shaatwibiy amesema hali ya kuyawekea maelezo maneno ya ImaamMaalik:

“Zingatia namna ambavo amezingatia kusimama kwenye jua, kuacha kuongea na kuweka nadhiri ya kwenda Shaam au Misri ni maasi, ingawa mambo hayo yenyewe kama yenyewe ni ya halali. Lakini pale yalipofanana na ´ibaadah, ndipo Maalikakayazingatia ni kumuasi Allaah.”[5]

[1] al-Bukhaariy 6704), Abu Daawuud (3300) naIbnMaajah (2136).

[2]Majmuu´-ul-Fataawaa (11/200).

[3]Majmuu´-ul-Fataawaa (11/614).

[4] al-Bukhaariy (3834).

[5] al-I´tiswaam (2/534).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 10/05/2023