23. Namna hii ndivo mambo ya halali yanakuwa Bid´ah

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuchukulia uvaaji wa vazi la pamba ni ´ibaadah na kujikurubisha kwa Allaah ni Bid´ah.”[1]

Kwa msemo mwingine imethibiti kuwa Bid´ah zinaingia katika mambo ya kiada kama ambavo zinaingia katika mambo ya ´ibaadah. Inafaa kuacha kula nyama, lakini mtu akiacha kula nyama kwa lengo la ´ibaadahbasi kitendo chake kinakuwa Bid´ah. ash-Shaatwibiy amesema:

“Bid´ah inatokea pale tu ambapo mzushi atafanya kitendo cha halali kwa kuamini kuwa kimewekwa katika Shari´ah ilihali ukweli wa mambo hakikuwekwa katika Shari´ah.”[2]

Vivyo hivyo kuvaa nguo kwa rangi maalum ni kitu kilichohalalishwa; lakini akivaa nguo ya rangi maalum kwa lengo la ´ibaadah inakuwa ni Bid´ah yenye kuchukiwa.

[1]Majmuu´-ul-Fataawaa (11/555).

[2] al-I´tiswaam.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 30
  • Imechapishwa: 10/05/2023