24. Qur-aan inawatahadharisha Ahl-ul-Bid´ah

Zipo dalili nyingi ndani ya Qur-aan, Sunnah na maneno ya Salaf zinazosimanga Bid´ah na kuzitahadharisha. Allaah (Ta´ala) amesema:

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ

“Yeye ndiye Aliyeteremsha kwako Kitabu – humo mna Aayah zilizo na maana ya wazi – hizo ndio msingi wa Kitabu – na nyinginezo zisizokuwa wazi maana. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotevu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitina na kutafuta kuzipindisha, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Ama wale waliobobea katika elimu husema: “Tumeziamini; zote ni kutoka kwa Mola wetu”, na hawakumbuki isipokuwa wale wenye akili.”[1]

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Aayah hiyo, ambapo akasema:

“Mkiwaona wale wanaofuata yale yasiyokuwa wazi basi tambueni kuwa hao ndio wale waliotajwa na Allaah. Hivyo basi tahadharini nao.”[2]

Maswahabah wengi – kukiwemo Ibn ´Abbaas na Abu Umaamah – wamehakikisha kuwa Khawaarih wanaingia ndani ya Aayah hii, kitu ambacho kinajulisha kuwa inawazungumzia Ahl-ul-Bid´ah.

[1] 3:7

[2] al-Bukhaariy (4547) na Muslim (2665).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 10/05/2023