Lau mtu angelipata mkabala kati yake yeye na mfalme wa kuonana mara tano kwa siku, angechukulia hilo kuwa ni sifa na angelifurahishwa na kitendo hicho na kutangaza ya kuwa kila siku anakutana na mfalme mara tano. Wewe unazungumza na Mfalme wa wafalme (´Azza wa Jall) kila siku mara tano kwa uchache. Ni kwa nini hufurahishwi na hilo? Mshukuru Allaah (´Azza wa Jall) kwa neema hiina simamisha swalah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/357)
  • Imechapishwa: 10/05/2023