Katika ukamilishaji wa kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah ni pamoja na kumsadikisha kwa yale aliyoeleza. Kila kilichosihi ni wajibu kwako kukisadikisha. Usishindishane nacho kwa kutumia akili na mtazamo wako. Ikiwa wewe huamini isipokuwa tu kile kinachokubaliana na akili yako, unakuwa sio muumini wa hakika. Wewe unafuata matamanio yako. Mtu ambaye anamuamini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kihakika anasema juu ya yale yaliyosihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Nimesikia, nimeamini na kusadikisha.”

Ama kusema “Vipi itawezekanaje?” huyu sio muumini wa kihakika.

Watu hawa ambao wanazihukumu akili zao juu ya yale aliyoelezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunakhofiwa juu yao. Ikiwa hawakubali isipokuwa yale yanayosapotiwa na akili zao, ijapokuwa akili zao ni finyu, ina maana hawakumuamini kihakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hawakuhushudia ya kuwa ni Mtume wa Allaah kwa njia inayotakikana. Shahaadah yao ni dhaifu kwa kiasi na wanavotilia shaka juu ya yale aliyoyaeleza.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/352 )
  • Imechapishwa: 09/05/2023