21. Namna hii ndivo mambo ya kiada yanakuwa Bid´ah

ash-Shaatwibiy (Rahimahu Allaah) ameunga mkono maoni yanayosema kuwa Bid´ah zinaingia ndani ya mambo ya ada kwa hoja nyingi, ikiwa ni pamoja na:

“Mambo ya kiada ni yenye kuzungumziwa na Shari´ahna ndani ya ile maana yenye kuenea ya ´ibaadah. Kwa ajili hiyo yaliyo halali ni moja ni moja katika hukumu za Shari´ah, kwa sababu imethibiti kuwa ni halali kwa dalili za Shari´ah. Imethibiti kwamba kila kitu ambacho kinahusiana na kuzungumzishwa kwa Shari´ah kinahusiana vilevile na Bid´ah.”[1]

Hoja nyingine ni:

“Wakati fulani mambo yaliyowekwa katika Shari´ah yanakuwa ´ibaadah na wakati mwingine yanakuwa ya kiada. Yote mawili yamewekwa katika Shari´ahna Mwekaji Shari´ah. Kama ambavoBid´ah zinaweza kutokea katika hicho cha kwanza, basi vilevile zinaweza kutokea katika hichi cha mwisho.”[2]

Hoja nyingine ni:

“Matendo ya watu wazima ima yakawa ni ´ibaadah au yakawa ni ya kiada. Kwa mujibu wa dalili za Shari´ah ni kwamba kila kitu cha kiada kinachohusiana na ´ibaadah kwa kiasi ya kule kufupilizika kwake na maamrisho ya Shari´ahkwa njia ya ulazima, ukhiyari au uruhusiwaji. Kwa msemo huyo ni kwamba Bid´ah zinaingia ndani ya mambo ya kiada kwa upande wa ´ibaadah uliofungamana nazo.”[3]

Haya ndio yaliyothibitishwa na ash-Shaatwibiy na akayawekea mlango wa kujitegemea katika kitabu chake “al-I´tiswaam” na ndio maoni yaliyosimama juu ya dalili na kusapotiwa na mwenendo wa Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Miongoni mwa dalili hizo ni yale aliyopokea Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Walikuja watu watatu nyumbani kwa wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakiwauliza kuhusu ´ibaadah zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati walipoelezwa, ni kana kwamba walizidharau na wakasema: “Vipi sisi tujilinganishe na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kwani yeye Allaah amemsamehe dhambi zilizotangulia na zinazokuja.” Mmoja wao akasema: “Hakika mimi nitaswali usiku mzima.” Mwingine akasema: “Mimi nitafunga daima na sintofungua.” Mwingine akasema: “Mimi najitenga na wanawake na kamwe sintooa.” Ndipo akaja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema: “Nyinyi ndio ambao mmesema hivi na hivi? Naapa kwa Allaah! Hakika mimi ni mwenye kumuogopa Allaah na kumcha zaidi kuliko nyinyi, lakini mimi nafunga na wakati mwingine sifungi, naswali na wakati mwingine nalala na naoa wanawake. Yule anayezipa mgongo Sunnah zangu basi si katika mimi.”[4]

[1] al-I´tiswaam (1/60).

[2] al-I´tiswaam (2/562).

[3] al-I´tiswaam (2/570).

[4] al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1052).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 09/05/2023