Mke anatakiwa ikiwa ni pamoja na kutimiza sharti tano:

1- Anatakiwa kuwa mzuri.

2- Awe ni mwaminifu wakati mume anapokosekana na anapokuwepo.

3- Asiwe ni mwenye kutazama wanaume wengine.

4- Asiwe ni mwenye kwenda kwenye masoko.

5- Asiwe ni mzungumzaji sana.

Ikiwa sharti moja itakosekana, sio mwanamke mwema kwa Muislamu kumuoa.

Sifa hizi imekuwa ni nadra kupatikana leo. Hii ni kwa sababu wanawake wengi wameacha maadili ya kidini. Ni kutokana na kwamba mafundisho ya mwanamke hayakutiliwa vigezo. Ghafla wakuta madhumuni ya kusoma ni kutaka ajira. Ajira inawaathiri wanawake katika njia tofauti. Isitoshe anapata vilevile ulimi mrefu. Anachukulia sahali kuwaangalia wanaume na kuchanganyika pamoja nao. Hili makafiri wamelisimamia nyuma kwa madai ya kumtakia uhuru mwanamke na kusema kwamba ni demokrasia na kwamba mwanamke anatakiwa kuwa kama mwanaume na kwamba Uislamu unawakandamiza wanawake.

Hivi kuna eaislamu ambao wana mawazo kama haya na wanalingania kwenye mawazo hayo, ambayo huletwa katika baadhi ya magazeti na suhuf. Wanataka mwanamke apande juu dhidi ya maandiko ya kidini. Kwa ajili hiyo ndio maana ni nadra wanawake kuwa na sifa hizi. Hili ni katika udadisi na mitihani mikubwa ya Uislamu na ni mfano wa jinsi waislamu walivyoathirika na propaganda na upotevu wa makafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ittihaaf-ut-Twullaab, uk. 873-874
  • Imechapishwa: 19/09/2020