Swali: Nafanya kazi na nafunga Ramadhaan na Saudi Arabia. Wakati niliposafiri kwenda katika nchi yangu swawm ilizidi siku moja juu ya swawm ya Saudi Arabia na hivyo funga yangu ikawa siku thelathini na moja. Je, nifunge au nile siku hiyo ambayo niko katika mji wangu?

Jibu: Funga pamoja nao na ufungue pamoja nao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fungeni siku wengine wanafunga.”

Ukifika katika mji wako basi utafunga pamoja nao mwezi uliobakia hata kama wamezidi kwa siku moja. Lakini haifai ikiwa ni kwa kupungua mwezi. Kwa sababu mwezi haupungui siku ishirini na tisa. Lakini kama umefika wakafunga kwa kuzidisha, kwa sababu walichelewa kuanza na ile nchi ulipokuwepo, basi funga pamoja nao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Fungeni siku wengine wanafunga, fungueni siku wanayofungua na chinjeni siku wanayochija.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023