Maoni ya Ibn Baaz kwamba kila watu wa nchi na mwandamo wao

Swali: Kila mwaka kunakuwa na mkanganyiko kuhusu mwezi wa Ramadhaan wakati wa kuanza na wakati wa kumalizika kwake ambapo inatofautiana miji ya waislamu kati ya wanaotangulia na wanaochelewa. Ni upi ufumbuzi wa tatizo hili?

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Kila watu wana mwandamo wao. Jambo ni lenye wasaa. Kama alivosema Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wakati Kurayb alipofika Madiynah kutoka Shaam ambapo Ibn ´Abbaas akamuuliza:

“Mu´aawiyah na watu wa Shaam wamefunga kwa kitu gani?”Akasema: “Wamefunga siku ya ijumaa. Watu wameuona siku ya ijumaa ambapo Mu´aawiyah akafunga na watu nao wakafunga.”Ibn ´Abbaas akasema: “Sisi tumeuona siku ya jumamosi. Hivyo tutaendelea kufunga mpaka tukamilishe mwezi au tuone [mwezi mwandamo].”

Akaona kuwa Shaam ni mbali na kwamba mwandamo wa watu wa Shaam hauwalazimu wakazi wa Madiynah. Jopo la wanazuoni wameshika maoni hayo. Kikosi cha wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wanaona wakazi wa kila mji wana mwandamo wao. Kwa hivyo wakazi wa Saudi Arabia wakiona mwezi mwandamo wakazi wa Shaam na Misri pia watafunga. Ni sawa pia ikiwa wataacha kufunga na wakafunga kwa mwezi mwandamo wao. Baraza la wanazuoni wakubwa wametoa fatwa hiyo ya kwamba ni sawa kwa kila watu wa mji na mwezi mwandamo wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023