Ibn Baaz kuhusu du´aa ya mwezi mwandamo

Swali: Du´aa inayosomwa wakati wa kuona mwezi mwandamo:

الله أكبر. اللهم أهله علينا بالأمن والإيمان. والسلامة والإسلام. والتوفيق لما تحبه وترضاه. ربي وربك الله. هلال خير ورشد

”Allaah ni mkubwa! Ee Allaah! Uanzishe kwetu kwa amani na imani, usalama na Uislamu, kutuwafikisha kwa yale unayoyapenda na kuyaridhia, Mola wetu na Mola wako ni Allaah. Mwezi mwandamo wa kheri na uongofu.”

imethibiti?

Jibu: Kuna unyonge katika cheni ya wapokezi wake. Mtu akiisema hapana vibaya – Allaah akitaka. Cheni yake imetiwa maneno. Kuna baadhi ya nyonge lakini hata hivyo hapana neno – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023