Kufungua kwa ambaye amesafiri kwa ndege saa moja kabla ya magharibi

Swali: Vipi kuhusu kalenda ambayo mfungaji anafungua kwayo wakati ndege inaporuka takriban saa moja na nusu kabla ya magharibi kutoka Riyaadh kwenda kwa mfano Cairo?

Jibu: Akianza safari kabla ya kuzama kwa jua bado ni mwenye kufunga mpaka jua lizame akiwa ndani ya ndege au akawa katika nchi ambayo tayari kwao jua limekwishazama. Hapo ndipo atafungua. Lakini akifungua katika mji ambao tayari jua limekwishazama kisha ndio akaanza safari ya ndege na ikaruka na akaona jua, haimdhuru. Katika hali hiyo atakamilisha swawm yake na haimdhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023