Swali: Upara ni pale ambapo sehemu fulani ya kichwa inaota zaidi…

Jibu: Ikiwa ni maumbile yake hakuna neno.

Swali: Lakini akikata sehemu za kandokando na akaacha upande ambao una kipara – kunaingia katika Qaz´?

Jibu: Asizifanye kitu.

Swali: Makatazo ni kwa njia ya uharamu?

Jibu: Ndio. Huu ndio msingi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninayokukatazeni basi jiepusheni nayo na nikikuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”

Amesema (´Azza wa Jall):

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni.”[1]

Hii ndio kanuni kwa wanazuoni; ya kwamba msingi wa makatazo ni uharamu na msingi wa amri ni ulazima. Isipokuwa pakiwepo dalili.

[1] 59:07

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21942/حكم-قص-جوانب-الراس-وترك-جهة-الصلع
  • Imechapishwa: 07/10/2022