Swali: Kufuga nywele.

Jibu: Ni sawa ikiwa ndani yake hakuna uharibifu. Lakini akizifuga kwa lengo la uharibifu, kuwawinda wanawake na machafu ni haramu. Hata hivyo hapana neno akizifuga kwa ajili ya Sunnah na kwamba amekusudia kheri na Sunnah.

Swali: Nywele ndefu kwa wanamme ni Sunnah?

Jibu: Akizifuga kwa nia njema na nia yake si kucheza na kueneza maharibifu ardhini.

Swali: Ni Sunnah?

Jibu: Itafaa.

Swali: Azirefushe urefu wa wazi?

Jibu: Hakuna kikomo maalum. Lakini malengo yake yasiwe mabaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/ما-حكم-اتخاذ-الشعر-واطالته
  • Imechapishwa: 07/10/2022