Peponi hakuna ´ibaadah

Swali: Je, watu Peponi watasema “Subhaan Allaah” na “Allaahu Akbar” kwa njia ya ´ibaadah?

Jibu: Watamsabihi Allaah kwa njia ya neema. Wataburudika kwayo. Kila mmoja atakuwa na wake wawili wa Peponi (الحور العين) mbali na wale wakeze wa duniani. Kila mmoja Peponi atapewa wake wawili wa Peponi mbali na wakeze. Kwa maana nyingine mtu hatokuwa na chini ya wake wawili wa Peponi ukiongeza na wale wakeze wa duniani pamoja na wake wengine ambao Allaah atampa mtu.

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa Peponi kuna ´ibaadah?

Jibu: Hakuna ´ibaadah. Ni nyumba ya starehe. Kusema “Subhaan Allaah” ni burudisho wanastarehe kwayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22738/هل-في-الجنة-تكليف-مثل-التسبيح-والتكبير
  • Imechapishwa: 12/08/2023