Ibn Baaz kuhusu kutumia Hadiyth dhaifu

Swali: Je, mtu afanyie kazi Hadiyth ambayo ni dhaifu upande wa cheni yake ya wapokezi lakini maana yake ni sahihi?

Jibu: Inafanyiwa kazi ikiwa na dalili. Dalili ni yale yanayofahamishwa na Qur-aan na Hadiyth Swahiyh.

Swali: Shaykh Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) anasema kuwa Hadiyth dhaifu imejengeka juu ya dhana na kwa ajili hiyo yeye haoni kufaa kufanyiwa kazi kwa sababu imejengeka juu ya dhana na kwamba dhana ndio mazugumzo ya uwongo kabisa.

Jibu: Hapana. Hadiyth dhaifu inafanyiwa kazi katika mambo ya kuhimiza na kuogopesha na inatumiwa katika mambo ambayo kumethibiti msingi wake.

Swali: Ameyarudisha hayo na kusema kuwa Hadiyth ambazo ni Swahiyh zimejaa katika chuo cha kuhimiza na kuogopesha na kwa ajili hiyo zinatosheleza.

Jibu: Haina neno. Zinatajwa katika chuo cha kuhimiza na kuogopesha. Mtu aseme kuwa inasemekena kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema… ndivo walivosema wanazuoni. Kwa kuashiria pasi na kukata.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22736/هل-يعمل-بالحديث-الضعيف-لو-صح-معناه
  • Imechapishwa: 12/08/2023