“Wewe ni katika watu wa Peponi – Allaah akitaka”

Swali: Baadhi ya watu wanamwambia mtu mwema kuwa ni katika watu wa Peponi – Allaah akitaka. Je, kuna ubaya wowote kusema hivo?

Jibu: Bora ni yeye kusema “Nataraji utakuwa katika watu wa Peponi”. Vinginevyo hapana vibaya maadamu amesema “Allaah akitaka”. Hata hivyo bora ni kusema  “Nataraji utakuwa katika watu wa Peponi”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22740/هل-يجوز-الحكم-للرجل-الصالح-بالجنة
  • Imechapishwa: 12/08/2023