Swali: Je, mtu alaze nia ya swawm usiku?

Jibu: Lazima:

“Kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia.”

Kila siku ina nia yake. Siku ni yenye kujitegemea. Haya ndio maoni sahihi.

Swali: Akiamka kwa ajili ya daku?

Jibu: Akiamka kwa ajili ya daku ndio ameweka nia ya kufunga.

Swali: Vipi ikiwa mwanzoni mwa mwezi ataweka nia moja?

Jibu: Haitoshi. Maoni sahihi ni kwamba ni lazima aweke nia kila siku. Akifunga ilihali ameghafilika pasi na kunuia kitu, haisihi. Ni lazima aweke kila siku kwa sababu kila siku ni yenye kujitegemea. Akila siku moja wapo amefungua. Akifanya tendo la ndo amefungua. Kila siku ni yenye kujitegemea.

Swali: Akisahau?

Jibu: Inatosha muda wa kuwa usiku alinuia atafunga kesho. Muda wa kuwa amenuia kuwa kesho atafunga inasihi licha ya kwamba hakukumbuka wakati wa daku.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22785/متى-وكيف-يكون-تبييت-نية-الصوم
  • Imechapishwa: 23/08/2023