Duu´a ambazo hazikupokelewa katika Sujuud?

Swali: Vipi kuhusu kuomba du´aa ambazo hazikupokelewa katika Sujuud?

Jibu: Aombe kile anachotaka katika du´aa nzurinzuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake anapokuwa amesujudu. Hivyo aombeni du´aa kwa wingi.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake anapokuwa amesujudu. Hivyo basi, jitahidini katika du´aa.”

Swali: Bora si aombe du´aa zilizopokelewa?

Jibu: Sio lazima. Bora aombe yaliyopokelewa na ni sawa akiomba du´aa zingine. Watu wana mahitaji yao. Kwa hivyo ni sawa akiomba du´aa zilizopokelewa au akaomba du´aa nyenginezo.

Swali: Si jambo linalopingana na Sunnah?

Jibu: Haliendi kinyume na Sunnah. Aombe yale ambayo Allaah amemsahilishia.

Swali: Je, si imepokelewa kwamba achague katika du´aa zinazopendeza zaidi kwake?

Jibu: Hili ni kuhusu mwishoni mwa swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafunza Maswahabah baada ya Tashahhud kwa kusema:

“Kisha achague katika du´aa inayopendeza zaidi kwake.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Kisha achague katika mambo anayoyapenda mwishoni mwa swalah.”

Vivyo hivyo kuhusu du´aa katika Sujuud. Hukumu yake ni moja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22790/هل-يجوز-الدعاء-في-السجود-بغير-الوارد
  • Imechapishwa: 23/08/2023