Swali: Kujivua katika ndoa (الخُلْع) ni kitu gani?

Jibu: Kuachika kwa kutoa pesa. Huku ndio kujivua. Yule mwanamke anampa pesa ili aweze kumwacha. Kunaitwa kujikomboa. Mwanamke anapotaka kujivua anampa pesa na baada ya hapo akakubali kumwacha, huku ndio kujivua katika ndoa. Inaitwa vilevile talaka juu ya fidia. Ni jambo lilitokea wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwanamke wa Qays alijivua kwake baada ya mgororo uliopitika kati yao. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

“Utamrudishia shamba lake?” Akasema: “Ndio.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia Thaabit: “Kubali shamba na mtaliki.”

Huku ndio kunaitwa kujivua. Ndio kilichokusudiwa katika maneno Yake (Ta´ala):

فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا فِيمَا افْتَدَتْ بِهِ

”… basi hakuna neno juu yao katika ambacho amejikombolea kwacho.”[1]

[1] 02:229

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23013/ما-معنى-الخلع-وكيف-يتم
  • Imechapishwa: 16/10/2023