Swali: Wakati ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alipotaka kuoa mwanamke mwingine juu ya bibi Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa), Mtume wa  Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

“Mke ana haki zaidi ya kujivua katika ndoa.”

Je, ni sahihi?

Jibu: Si sahihi. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]

Kuhusu kisa cha Faatwimah ni maalum kinachomuhusu Faatwimah peke yake. Wakati ´Aliy alipotaka kumuoa msichana wa Abu Jahl, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

“Hakusanyiki msichana wangu na msichana wa Abu Jahl, kwani yananiudhi yale yanayomuudhi yeye na pia yeye ni sehemu yangu.”

Hili ni jambo maalum kwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Vinginevyo kuoa wake wawili, watatu na wanne ni jambo linalofaa. Mke wa kwanza hana haki ya kupinga; isipokuwa ikiwa kama alimuwekea sharti mwanaume asioe mwanamke mwingine juu yake. Katika hali hiyo itambulike kuwa waislamu wanatakiwa kutimiza masharti waliyowekeana. Lakini kama anataka kuoa, kufanya uadilifu na asimamie majukumu yake, ni sawa akaoa wake wawili, watatu au wanne.

[1] 04:03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23012/خصوصية-عدم-الزواج-على-بنت-النبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 16/10/2023