Swali 50: Kipi kilitokea mwaka wa tano?

Jibu: Katika mwezi wa Rabiy´ al-Awwal vita vilianza karibu na Dawmat-ul-Jandal.

Mwaka huohuo katika Shawwaal, ulikuwa ni wakati wa vita dhidi ya wale waliokula njama, kisha dhidi ya Banuu Quraydhwah ambao walikubali kuhukumiwa na Sa’d bin Mu’aadh. Aliwahukumu wapiganaji wanyongwe, wanawake na watoto wao wafanywe mateka na kuchukuliwa kwa mali zao. Kukateremshwa kuhusiana na tukio hilo kuanzia maneno Yake Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَةَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ جَاءَتْكُمْ جُنُودٌ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا وَجُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرًا

”Enyi walioamini! Kumbukeni neema ya Allaah juu yenu pale yalipokujieni majeshi tukawapelekea upepo wa dhoruba na majeshi msiyoyaona; na Allaah daima ni Mwenye kuyaona myatendayo.”[1]

mpaka:

وَأَوْرَثَكُمْ أَرْضَهُمْ وَدِيَارَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ وَأَرْضًا لَّمْ تَطَئُوهَا ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرًا

”Akakurithisheni ardhi yao na majumba yao na mali zao na ardhi hamkuwahi kuzikanyaga; na Allaah daima ni Muweza juu ya kila jambo.”[2]

[1] 33:9

[2] 33:27

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 114
  • Imechapishwa: 16/10/2023