Miongoni mwa mambo bora kutaja hapa ni yale ambayo Umm Ja´far bint Muhammad bin Ja´far ya kwamba Faatwimah, msichana wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), amesema:

”Ee Asmaa´! Hakika mimi nimechukizwa na yale yanayofanywa na wanawake wanapozikwa na nguo za kubana.” Asmaa´ akasema: ”Ee msichana wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Nisikuonyeshe kitu nilichokiona Uhabeshi?” Akaomba majani  mabichi ya mitende ambayo aliyakunja kisha akamrushia nguo. Faatwimah akasema: ”Ni nzuri iliyoje! Kwayo anatambulika mwanamke kutokamana na mwanamme.  Nitapokufa mimi, basi nioshe wewe na ´Aliy. Asiingie ndani yeyote.” Alipokufa ´Aliy na Asmaa´ (Radhiya Allaahu ´anhum) ndio waliomuosha.”[1]

Tazama namna ambavo Faatwimah, mboni ya jicho la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jinsi alivyochukizwa na nguo ya kubana ya mwanamke ilihali amekwishakufa. Ni jambo lisilokuwa na shaka kuwa machukizo ya nguo ya kubana ni mabaya zaidi na zaidi ikiwa zinavaliwa na wanawake waliohai. Wayazingatie haya wanawake wa Kiislamu wa leo ambao wanavaa nguo hizi zenye kubana zinazoonyesha maumbo ya vifua, viuno, makalio, miguu na viungo vyao vyengine vya mwili kisha wamuombe Allaah msamaha na watubu Kwake. Wakumbuke maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Hayaa na imani ni mambo yanaenda sambamba. Kinapoondoka kimoja, basi kinaondoka kingine.”[2]

[1] Abu Nu´aym katika ”Hilyat-ul-Awliyaa’” (2/43) na tamko ni la kwake na al-Bayhaqiy (4/34-35) kwa upokezi ambao umekamilika zaidi ambao humo imekuja ya kwamba Asmaa’ alimtengenezea Faatwimah jeneza kama alivyomweleza. 

[2] al-Haakim (1/22) na Abu Nu´aym (4/297) kupitia kwa Ibn ´Umar. al-Haakim ambaye amesema:

”Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.”

adh-Dhahabiy ameafikiana naye na mambo ni kama alivosema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 16/10/2023