Ni lazima unayemuhijia awe ameacha wasia?

Swali: Kuhusu ambaye anahiji kwa niaba ya mwingine si imeshurutishwa kwamba mtu huyo awe ameacha wasia?

Jibu: Hapana, hata kama hakuusia. Lakini ni sharti anayemfanyia awe tayari ameshajifanyia mwenyewe hajj. Anayemuhijia mwingine ni lazima awe ameshajihijia mwenyewe. Vivyo hivyo kuhusu kumfanyia mwingine ´Umrah; awe ameshajifanyia ´Umrah mwenyewe kwanza.

Swali: Vipi ikiwa mtu huyo alizembea?

Jibu: Hata kama alizembea. Ahijiwe na aombewe du´aa ya msamaha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22856/هل-يجب-ان-يوصي-من-يحج-عن-الغير
  • Imechapishwa: 29/08/2023