´Umrah ndani ya Ramadhaan kila mwaka

Swali: Mtu afanye ´Umrah katika Ramadhaan kila mwaka au inatosha mara moja tu?

Jibu: Akifanya kwa wingi kila mwaka ni bora. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“´Umrah katika Ramadhaan inalingana na hajj.”

Swali: Vipi ikiwa atakariri ndani ya Ramadhaan mara moja au mara mbili?

Jibu: Hakuna kizuizi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“´Umrah moja hadi nyingine ni kifutio cha madhambi kwa yale yaliyoko baina yake.”

Hakuweka kikomo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni sawa akifanya ´Umrah kila mwaka au kila baada ya miezi miwili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22850/هل-تستحب-العمرة-في-رمضان-كل-عام
  • Imechapishwa: 29/08/2023