02. Anavyoweza mwanamke kuonyesha kwa mtazamo wa at-Twabariy

Salaf wametofautiana katika kuifasiri. Wako waliosema ni ile nguo ya juu inayoonekana na wengine wakasema kuwa ni wanja, pete, bangili, uso na maoni mengine kutoka kwa baadhi ya Maswahabah na wanafunzi wao ambayo yametajwa na Ibn Jariyr katika tafsiri yake ya Qur-aan. Kisha yeye mwenyewe akachagua maoni ya kwamba kumebaguliwa uso na mikono[1]:

”Maoni yaliyo karibu zaidi na haki ni yale ya waliyovua uso na mikono. Mambo yakishakuwa hivo basi kunaingia pia wanja, pete, bangili na kujipaka rangi. Nimeyachagua maoni hayo kwa sababu wote wanaona kuwa ni lazima kwa mwanamme anayeswali kufunika viungo vyake vya siri wakati anaswali na kwamba inafaa mwanamke anayeswali kufunua mikono yake na kwamba viungo vyake vyengine vyote vya mwili vilivyosalia anatakiwa kuvifunika. Isipokuwa vile vilivyopokelewa[2] kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amemruhusu mwanamke anayeswali kuonyesha nusu ya mikono yake. Ikiwa wote wameafikiana juu ya hilo, basi hiyo ina maana kuwa inafaa kwake mwanamke, kama ilivyo kwa mwanaume, kuonyesha mwili wake yale ambayo sio viungo vya siri. Kwa sababu vile viungo visivyokuwa vya siri sio haramu kuvionyesha. Na ikiwa inafaa kwake kuonyesha vitu hivyo basi inatambulika kuwa hayo ndio yale yaliyobaguliwa na Allaah (Ta´ala) pale aliposema:

إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا

“… isipokuwa yale yanayodhihirika… “

Kwa sababu vyote hivyo ni vyenye kuonekana kwake.”[3]

[1] Mikono inakusanya viganja vya mikono mpaka kwenye kiwiko. Uso ni kuanzia kwenye maoteo ya nywele za kichwa mpaka chini ya kidevu na kuanzia sikio moja hadi sikio jingine. Hivo ndivo walivosema wanazuoni tofauti na baadhi ya watu wa leo. Wataraddiwa mwishoni mwa mlango huu.

[2] Ni kana kwamba Ibn Jariyr anaashiria kuwa Hadiyth ni dhaifu aliposema kuwa imepokelewa. Ana kila haki ya kufanya hivo. Tamko kama hilo si Swahiyh. Naona Hadiyth hiyo kwanza ni dhaifu, pili inapingana na Hadiyth zilizo Swahiyh. Ameipokea Ibn Jariyr kupitia kwa Qataadah ambaye amesema…

[3] Jamiy´-ul-Bayaan (18/84).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 29/08/2023