37. Kama kuna yeyote angesalimishwa na kifo…

Mashairi haya, yanayoashiria msiba ulio wazi na mkubwa, nao ni kifo cha bwana wetu, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), yamenikumbusha ubeti niliyosoma hapo kitambo. Nayafanya ndio yenye kumalizia kitabu hiki. Nayo ni kama ifuatavyo:

Maisha haya si jengine isipokuwa ni ndoto

kila mmoja atalijua wakati atakapoiaga dunia

Anasema ´laiti kama` na nini itasaidia

kwa sababu mauti yamekwishampiga kwa mishale yake

Anatamani lau angelibaki japo kitambo kidogo

 ili aweze kutubia juu ya utendaji madhambi

Ni vipi atatubia ilihali nafsi yake

Imeshakusanywa kwenye kifua chake, tayari kwa ajili ya kuondoka?

Enyi mliolala, amkeni! Mara nyingi yanaghurisha

maisha marefu ya duniani yanatangatanga

Huku wakiwa katika kughafilika

wanapigwa na kitu kinachowapooza na kuwaghafilisha

Wanawekwa ndani ya mashimo ambayo nyama zake hunyauka

na hakuna kinachobakia isipokuwa mifupa

Bali ni kwamba hata mifupa hupotea

ambayo nyuso zake zilikuwa ziking´aa gizani

Ni uzuri uliyoje ambao tulikuwa nao sote

baada ya kutuondoka, kunajitokeza upendo

Kila wanapotiwa mdomoni, shauku inaongezeka na shauku ikazidi

Kifo hiki ni cha Allaah na hakikusalimisha

si anayemcha kwa ajili ya uchaji wake wala mtenda dhambi

Endapo kingemsalimisha kiumbe yeyote

basi kingemsalimisha Mtume wa Allaah anayeheshimika

Lakini hata yeye amekunywa kwenye kikombe chake

licha ya kuwa yeye ni kipenzi cha Allaah, mbora wa viumbe

Matokeo yake ardhi ikajikusanya na kila aliye juu yake

na mawingu yakaanza kunyesha

Kila jicho likatiririka machozi na

machozi mepesi juu yake yakawa ni machozi ya furaha

Msikiti ukalia kutokana na kumpoteza

na vivyo hivyo nyumba ikalia kisha nguzo

Bali kila ardhi iliyoguswa na kuondoka kwake

baada ya nuru ikazama kwenye viza

Hakuna viumbe kama Maswahabah zake

wakati walipomuaga chini ya salamu hiyo

Wakageuka na kumuondokea,

wakiwa na huzuni na wasiweze kuongea

Kifo cha mteule ni msiba mkubwa –

wa Allaah usiofanana na mifupa

Kifo chake ni somo kubwa ambalo –

linawepesisha misiba ya wema na watu watukufu

Hata hivyo yuko hai na katika bustani kubwa la Njia

na katika cheo cha juu

Allaah amsifu kwa fadhilah Zake na amsalimishe milele

kisha jamaa zake, Maswahabah zake na wale Taabi´uun wema

Mpaka hapa kimemalizika kitabu ”Bard-ul-Akbaad ´an Faqd-il-Awlaad”. Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhamamd, kizazi chake na Maswahabah zake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 128-130
  • Imechapishwa: 29/08/2023