36. Kulia na kuhuzunika kwa Salaf

Kulikuja taarifa kwamba mtoto wa bwana mmoja anayetokana na kizazi cha ´Aliy, kutokea Twabaristaan, alifariki. Wakaja watu kumpa rambirambi, lakini hakukutana nao katika siku ya kwanza, siku ya pili wala siku ya tatu. Halafu baada ya hapo akawatokea na kuwaambia:

“Kufa kwa mwanangu si mwanzo wala mwisho. Wala hakikuishilia kwake. Lakini mimi nafikiria juu ya urefu wa huzuni yake katika kututoweka na urefu wa huzuni yetu juu ya kutoweka kwake na upweke wake.” Akalia kitambo fulani, kisha akasema:

Masikini mgeni katika nchi geni

nini alichofanya juu ya nafsi yake mwenyewe?

Amewaacha wapenzi wake na

hawakunufaisha na maisha baada yake na wala

Moyo wangu umejaa huzuni

na umekatika kwa sababu ya kutamani na umbali

Yuko mbali na peke yake

 na yote anayofanya Allaah ni uadilifu

Imepokelewa ya kwamba kuna mtu alisimama kwenye kaburi na akilia pamoja na wengine. Kisha akasema:

Ee kifo, ni ugumu kiasi gani, unapiga

Unampiga yule asiyetaka kupigwa

Unamchukua mwanamali kutoka chumbani kwake

na unamchukua mtu kutoka kwa mama yake

Humbakizi mwema wala muovu

isipokuwa unawapeleka kwenye makaburi yao

Hivo ndivo inavyokuwa hukumu ya Asiyeshindika, Mjuzi na Muweza

Ametakasika na mapungufu – hadhulumu katika hukumu Yake

Haafidhw Abu ´Abdillaah al-Haakim amepokea katika ”at-Taariykh” yake kupitia kwa Sa´iyd bin al-Musayyab, ambaye amesema:

“Tuliingia makaburi ya Madiynah tukiwa na ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Akasimama karibu na kaburi la Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Pindi watu walipoondoka, alisema:

Kila mkusanyiko wa wapenzi wawili hutengana

ubakiaji wangu baada yenu ni mdogo

Kumpoteza mmoja baada ya mwingine

kunajulisha kuwa hakuna mpenzi atakayedumu

Nayaona maradhi ya dunia kwangu ni mengi

Mwenye kuishi ni mgonjwa mpaka wakati wa kufa

Abu Muhammad ´Abdur-Rahmaan bin ´Umar bin an-Nahhaa amepokea kutoka kwa Muhammad bin Sulaymaan, ambaye amesimulia kuwa al-´Atabiy amesema:

“Baada ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kumaliza kumzika Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa), msichana wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akarudi na huku akisema:

Kila mkusanyiko wa wapenzi wawili hutengana

ni wachache ambao bado hawajakufa

Kumpoteza mmoja baada ya mwingine

kunajulisha kuwa hakuna mpenzi atakayedumu

Nayaona maradhi ya dunia kwangu ni mengi

Mwenye kuishi ni mgonjwa mpaka wakati wa kufa

al-´Atabiy ameeleza kuwa adh-Dhwabbiy alisoma mashairi ya al-´Atwannash na akasema:

Baada ya kulia mito ya machozi nasema

kwamba naona ardhi inabaki na marafiki wanaondoka

Marafiki zangu! Ningekata tamaa lau kilichowapa kingekuwa kingine kisicho kifo

lakini kifo hakiepukiki

Kuna mifano mingi ya namna ambavyo Salaf walilia wakati wa kuwapoteza watu na kusoma mashairi katika kipindi cha kutamani. Bora, nzuri, kweli na inayopigiwa mfano zaidi katika maudhui haya, ni yale Ja´far bin Muhammad aliyosimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

“Wakati lilipofunikwa udongo kaburi la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam), alikuja Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambapo akachukua udongo kutoka kwenye kaburi na kuuweka machoni mwake. Akalia na kusema:

Ni kwa nini yule ambaye amenusa udongo wa Ahmad

asinuse urefu hadhi ya wakati?

Lau michana ingelipatwa na masaibu yangu

basi ingelikuwa nyusiku[1]

Abu Bakr Muhammad bin al-Husayn al-Aajurriy amesema katika ”ash-Shariy´ah”:

“Nimefikiwa na khabari kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) alipomaliza kuzikwa, alikuja Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwenye kaburi lake na kusema:

Machozi kwenye mashavu yangu yameanguka chini

kwa ajili ya kukusitikia – moyo umejaa madonda

Ni vizuri daima kuwa na subira

isipokuwa inapohusu wewe – ni jambo haliwezekani

Hakuna aibu ya kukuhuzunikia –

kama huzuni ingekuwa ni kwa aina ya kilio cha milele machoni mwangu

[1] adh-Dhahabiy amesema:

“Haya ni katika yaliyonasibishwa kwa Faatwimah lakini hayakusihi.” (Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (2/134)).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 125-128
  • Imechapishwa: 29/08/2023