21. Hadiyth “Hakika si vyenginvyo swalah ni kama mfano wa mto wa maji matamu… “

371 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

كان رجلان أخوان، فَهَلَكَ أحدُهما قبل صاحبه بأربعين ليلة، فَذُكِرَتْ فَضيلةُ الأولِ منهما عند رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -، فقال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ”  ألم يكن الآخر مسلماً؟.

قالوا: بلى، وكان لا بأس به. فقال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ”  وما يدريكم ما بَلَغَتْ به صلاتُه؟ إنَّما مُثّل الصلاةِ كمثَل نهرٍ عَذْبٍ غَمْرٍ، ببابِ أحدِكُم، يَقْتَحِم فيه كلَّ يوم خمسَ مرات، فما تَرَون في ذلكَ يُبقي من درنه؟ فإنّكم لا تدرون ما بلغتْ به صلاتُه

“Walikuwepo ndugu wawili ambapo mmoja wao akafariki nyusiku arobaini kabla ya mwengine. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatajiwa fadhilah za yule wa kwanza, ambapo akasema: “Je, kwani yule mwingine hakuwa muislamu?” Wakasema: “Bila shaka, na hakuwa na neno.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Mnajuaje swalah yake imemfikisha wapi? Hakika si vyenginvyo swalah ni kama mfano wa mto wa maji matamu nje ya mlango wa mmoja wenu. Kila siku anajitupa humo mara tano. Hivi kweli mnaona kuwa atabaki akiwa na uchafu wowote? Hakika nyinyi hamjui swalah yake imemfikisha wapi.”[1]

Ameipokea Maalik, na tamko ni lake, na Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri, an-Nasaa´iy na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake, isipokuwa tu humo amesema:

كان رجلان أخَوان في عهدِ رسولِ الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -، وكان أحدُهما أفضلَ من الآخر، فتُوفِّي الذي هو أفضلُهما، ثم عُمِّر الأخرُ بعده أربعين ليلةً، ثم توفّي، فذُكر ذلك لرسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ – فقال:”  ألم يكن يصلي؟. “

قالوا: بلى يا رسول الله! وكان لا بأس بهِ، قال رسول الله – صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ”  وماذا يدريكم ما بلغت به صلاتُه

“Walikuwepo ndugu wawili wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambapo mmoja wao alikuwa mbora kuliko mwingine. Yule aliyekuwa mbora akafariki. Kisha yule mwingine akaishi zaidi kwa nyusiku arobaini. Baadaye akafariki. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatajiwa hayo, ambapo akasema: “Je, hakuwa anaswali?” Wakasema: “Bila shaka, ee Mtume wa Allaah. Hakuwa na neno. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ni kipi kinachokujuzeni swalah yake imemfikisha wapi… “[2]

[1] Swahiyh.

[2] Tamko hili lipo kwa Ahmad (1534).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/272)
  • Imechapishwa: 29/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy