Ni lazima kwa wanawake hawa kufunga na haitoshi kulisha chakula

Swali: Kuhusu mwanamke ambaye amekula Ramadhaan katika hali ya nifasi, ujauzito au unyonyeshaji na afya yake ni nzuri – je, bora ni kufunga au inatosha kumtolea swadaqah?

Jibu: Ni lazima kwa ambaye amekula mwezi wa Ramadhaan kwa sababu ni mwenye damu ya uzazi kulipa zile siku alizokula katika kipindi hicho. Kuhusu mjamzito analazimika kufunga kipindi cha ujauzito wake. Isipokuwa kama anachelea juu ya nafsi yake mwenyewe au kipomoko chake ikiwa kama atafunga. Katika hali hiyo ataruhusiwa kula na baadaye atalipa baada ya kujifungua na kusafika kutokamana na damu ya uzazi. Sambamba na hilo hatolazimika kulisha chakula pia ikiwa atalipa siku zake kabla ya kufikiwa na Ramadhaan nyingine. Kulisha hakumtoshelezi kutokamana na kufunga. Bali ni lazima afunge na kufanya hivo kutamtosheleza kutokamana na kulisha chakula.

  • Mhusika: al-Ladjnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ladjnah ad-Daaimah (10/226) Fatwa nr. (12591)
  • Imechapishwa: 19/04/2022