Utashangazwa na watu wengi pale tu inapoingia Ramadhaan basi wanajaa misikitini na wanachunga vipindi vya swalah. Kisha inapotoka Ramadhaan wanayaacha mambo hayo au mengi yake. Utaona katika baadhi ya nyakati, kama mfano wa swalah ya Fajr, safu haijai. Lakini unapokuja katika swalah ya Fajr mchana wa Ramadhaan basi utaona safu mbili au tatu. Je, hivi watu hawa walikuwa wafu na wakapatikana katka mwezi wa Ramadhaan au walikuwa wamesafiri halafu wakaja katika wezi wa Ramadhaan? Hawahifadhi swalah ya Fajr pamoja na mkusanyiko isipokuwa tu katika mwezi wa Ramadhaan. Wako wapi katika kuihifadhi ´ibaadah hii katika miezi yote?

Kwa ajili hiyo nasema: ambaye Allaah (´Azza wa Jall) amemtunuku, akamneemesha kuhifadhi vipindi vya swalah, moyo wake ukatikisika juu ya utiifu na ´ibaadah na akahisi ladha yake katika mchana wa Ramadhaan basi hiyo ni fursa kwa yeye kuendeleza mwenendo huo katika maisha yake yote ili aweze kufaidika kutoka katika mwezi wake mtukufu na katika msimu wake wenye kubarikiwa ili ahakikishe maana ilioko katika Aayah tukufu:

كتب على الذين من قبلكم لعلكم تتقون

“Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah.”[1]

Bi maana ili muweze kumcha Allaah (´Azza wa Jall) kupitia yale matendo mema na ´ibaadah mnazotekeleza katika msimu huu mtukufu.

[1] 01:183

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 20/04/2022