Swali: Utawaona watu wengi wakati wa mazishi wamekusanyika pembezoni mwa kaburi na wakizungumza. Hakuna utulivu wala faida ya kuhudhuria kwenye mazishi. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Huku ni kwenda kinyume na Sunnah. Katika hali kama hii mtu anatakiwa kufikiria mwisho wake na kusubiri kitachomfika na kujua kuwa mwisho wake ni kama walivyo maiti hawa. Hivi ndivyo inatakiwa kuwa hali ya mtu. Haitakiwi kuvutana wala kunyanyua sauti katika hali hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/169)
  • Imechapishwa: 25/08/2021