Ni ipi hukumu ya kulijengea kaburi ukuta ili kulilinda na wanyama?

Swali: Kuna kaburi lililo nje ya mji ambalo kumeota mti juu yake. Ngamia inakuja kula kwenye mti huu na kulikanyaga kaburi kwa ajili hiyo wakawa wamelijengea kaburi hili ukuta. Je, inajuzu?

Jibu: Mti huu unatakiwa kukatwa kuanzia kwenye mizizi. Tukifanya hivo ngamia haitorudi na kwa ajili hiyo tutakuwa tumesalimika na shari yake. Kaburi linatakiwa kubaki kama lilivyo. Kujenga ukuta kwa ajili ya kulihifadhi inaweza kupelekea huko mbeleni watu wakaanza kufikiria kuwa alikuwa ni katika mawalii au mja mwema. Tahamaki nchi hii ije kufikwa na matatizo ya makaburi baada ya Allaah kuisafisha kupitia Imaam Muhammad bin ´AbdilWahhaab (Rahimahu Allaah).

Hivyo ni lazima kumfikishia khabari Qaadhiy kuhusu suala hilo na khaswa ikiwa kama utengenezaji uko kama chumba. Ni lazima uondoshwe. Ikiwa kaburi linakhofiwa basi lihamishwe kwenda sehemu nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/204)
  • Imechapishwa: 25/08/2021