Ni ipi hukumu ya kujenga nyumba juu ya makaburi ya waislamu?

Swali: Nilirithi nyumba kutoka kwa marehemu mamangu. Nyumba ilibomolewa na kuboreshwa. Pembezoni mwake kumepatikana makaburi mengi. Pindi tulipokuwa tunachimba msingi wake tulipata mifupa iliyokwishaoza ambayo pengine ni ya yale makaburi yaliyo pembezoni na nyumbani. Nikachukua mifupa hii na kuizika sehemu ya mbali na nyumba. Nyumba imemalizwa kuboreshwa lakini imezungukwa na makaburi. Tumeirithi nyumba hii kutoka kwa mababu zetu na hatuna nyumba nyingine wala ardhi ya kujenga. Je, tuna haki ya kuishi kwenye nyumba hii? Je, nina dhambi kwa kuhamisha mifupa hii sehemu nyingine?

Jibu: Ikiwa makaburi haya ni ya waislamu, basi wao wana haki zaidi ya ardhi hii kuliko nyinyi. Pindi walipozikwa ndani yake wakawa ni wenye kuyamiliki. Haifai kwenu kujenga nyumba yenu juu ya makaburi. Ikiwa mna uhakika kuwa mmejenga juu ya makaburi, basi ni wajibu kwenu kuliondosha jengo hilo na kusiwepo jengo lolote juu ya makaburi. Kusema kwamba hamna nyumba nyingine haina maana sasa mdio mchukue nyumba za waislamu wenzenu. Makaburi ni nyumba za maiti. Msiishiemo ilihali mnajua kuwa watu wamezikwa ndani yake.

Kuhusu neno ´marehemu mamangu`, yanakemewa na baadhi ya watu kwa kuwa hatujui kuwa maiti huyu ni katika wenye kurehemewa au sio katika wenye kurehemewa. Makemeo haya ni ya sawa ikiwa mtu huyu anakusudia kuwa maiti huyu amerehemewa. Haifai kwake kusema kuwa amerehemewa au ameadhibiwa bila ya ujuzi. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلاَ تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْؤُولاً

“Na wala usiyafuate yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo, vyote hivyo vitaulizwa.”[1]

Lakini hata hivyo watu hawakusudii kueleza kwa kukata. Pindi watu wanaposema kwa mfano marehemu baba, marehemu mama au marehemu dada, hawamaanishi kukata moja kwa moja. Wanachokusudia ni kuwaombea Allaah (Ta´ala) awarehemu. Kuna tofauti kati ya du´aa na kuelezea. Kwa ajili hii ndio maana tunasema:

رحمه الله

“Allaah amrehemu fulani.”

غفر الله له

“Marehemu fulani.”

Kwa mujibu wa lugha ya kiarabu hakuna tofauti kati ya neno ´mrehemewa` na ´Allaah amrehemu fulani`. Pindi tamko moja litakatazwa basi inatakiwa vilevile kukataza lingine.

Ninaonelea kuwa tamko “marehemu fulani” na “msamehewa fulani” lisikemewe. Kwa kuwa hatuelezei kuwa Allaah amemrehemu au Allaah amemsamehe, bali tunamuombea kwa Allaah na kutarajia hivo. Yanasemwa kwa njia ya matarajio na du´aa na sio kwa njia ya kuelezea. Kama tulivyosema kuna tofauti kati ya hayo mawili.

[1] 17:36

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/205-207)
  • Imechapishwa: 25/08/2021